Header Ads

Bastian Schweinsteiger : Hi ni Zaidi ya Dharau.

Maisha yanazidi kuwa magumu ndani ya Manchester united kwa kiungo wa kimataifa kutoka nchini Ujerumani Bastian Schweinsteiger baada ya kuambiwa na club yake kwamba hana nafasi ndani ya Manchester united.Kiungo huyo aliyejiunga msimu uliopita ameambiwa hana hata nafasi ya kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza hivyo amelazimishwa kufanya mazoezi na kikosi cha akiba.

Kaka wa mchezaji huyo Tobias Schweinsteiger amesema Kocha wa Manchester united Mreno Jose Morinho amemkosea kabisha heshima Bastian kwa kitendo anachomfanyia.
Bastian Schweinsteiger ameambiwa hana nafasi kabisa ndani ya manchester united.

Wakati mchezaji mmoja wa timu ya kwanza ya Man chester united alipomuona Bastian katika vyumba vya kubadilishia nguo vya wachezaji wa mnchester united chini ya miaka 21 wiki kadhaa zilizopita alimuuliza ,unafanya nini huko!
Ni swali ambalo mshindi huyo wa kombe la dunia anajiuliza kila siku.Mchezaji ambaye ameshinda kombe la Bondasiliga mara nane amejikuta anashindwa hata kupata muda wa kusalimiana na Wayne rooney na Zlatan inapofika asubuhi na hatimaye ameishia kukutana na wachezaji wa kikosi cha watoto cha Man chester united.
Siku ya Alhamis,July 28,Schweinsteiger alifika kataika uwanja wa Mazoezi wa Carington ndipo alipata taarifa ya kwamba club haina mpango nae tena.

Mshindi wa kombe la Dunia,alipigwa picha hii msimu uliopita,kwa sasa anafanya mazoezi na wachezaji wa akiba Man united.


Kocha wa Machester united Jose Mourinho ambaye anatuhumiwa kwa kutomuonyesha heshima Bastian.


Meneja wa Manchester united Jose Mourinho amemwambia Mjerumani huyo kwamba hana nafasi tena ndani ya Manchester united hivyo amwambie wakala wake amtafutie timu nyingine.

Nafasi pekee aliyopewa mjerumani huyo ni kufanya mazoezi ya kujiweka vizuri wakati akiwa anatafuta timu nyingine.Na hali hii imetokea kwa Bastian baada ya ujio wa kocha huyo mreno ndani ya Manchester united.






No comments

Powered by Blogger.