Header Ads

Mke wa Raisi Magufuli Alazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

        Pichani Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli akimjulia hali mkewe katika hospitali ya  Muhimbili

Leo Novemba 10,2016 Ikulu imeweka picha ya Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania John Magufuli akiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhumbili Wodi ya Sewahaji ambako alikwenda kumuangalia mke wake Mama Janeth Magufuli aliyelazwa hapo.

Pamoja na kwenda kumuangalia Mkewe Raisi pia aliwaangalia wagonjwa wengine akiwemo Balozi mstaafu wa Tanzania  Omar Ramadhan Mapuri..

Baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika wodi ya Sewa Haji wamemshukuru "kwa hatua zilizochukuliwa na serikali kuboresha hospitali ya taifa ya Muhimbili na wamebainisha kuwa licha ya kuboreshwa kwa mazingira ya hospitali, pia wanapata huduma nzuri kutoka kwa madaktari na wauguzi.




No comments

Powered by Blogger.