Header Ads

Samsung na Panasonic watuhumiwa kunyanyasa wafanya kazi wao nchini Malaysia.

                                 Mtu Akitembea Jirani na ofisi za Samsung zilizopo kuala Lumpur Malaysia.

Wafanyakazi waliotoka nchi za mbali na kwenda kufanya kazi Malaysia katika kampuni za Samsung na Panasonic wamelalamika wakizituhumu kampuni zao kuwanyanyasa pamoja na kuwanyonya maslahi yao wanapokuwa kazini.

Samsung na Panasonic kampuni kubwa zinazoongoza kwa utengenezaji wa vifaa nya umeme duniani wanakabiliwa na tuhuma za unyanyasaji dhidi ya wafanya kazi wao.

Makampuni mawili yameanzisha uchunguzi kuhusu madai yaliyootolewa na wafanyakazi wao wanaotokea nepal .Mfanya kazi mmoja alisema "Walikuwa wakidanganywa kuhusu malipo na walipokonywa hati zao za kusalfilia na walipokuwa wakiomba kurudi kwao Nepal walilazimishwa kulipa faini kubwa sana".Walisema pia walilazimishwa kufanya kazi hadi masaa 14 kwa siku .

No comments

Powered by Blogger.